Saturday, April 28, 2012

MATATIZO YA KUTUMIA MAFUTA YA KUKAANGIA KWA KURUDIA -RUDIA

Mafuta yana ubora gani?
Tunapenda kukaanga vyakula vyetu.. Tunaongezeka uzito mara nyingi sana. Vyakula hivi ni vizuri, tunaongeza chumvi lakini lazima tutambue ni vyakula vya hatari sana. Kwani ni vyakula vya mazoea vilivyo sheheni kila kona ya mitaa yetu na majumbani mwetu.
Mafuta ya kupikia nini?
Mafuta ya kupikia ni muunganiko wa glycerol na acid za mafuta. Yanaweza kuwa na ni mafuta ya mimea, kama vile sunflower,pearnut, canola ama kutoka kwa wanyama. Utayarisha wa mafuta haya inategemea utayarisha wa mafuta haya kwani kuna njia nyingine ni za kitamaduni-kienyeji na hatua nyingine ni viwandani.
Kitu gani kinatokea mafuta yanapopikwa kwa muda mrefu?
Kuchemsha mafuta yakupikia mpaka kufikia joto la 170-220ºC (338-428ºC). inapochemshwa ukiwepo na hewa ya oksjeni, mafuta haya yanfanya kemikali kama vile za hydrolysis, oxidation, na polymerization(unachangia uwepo wa kutu), kwa maana nyingine yana badilika tabia yake, uzito wa mafuta unaongezeka rangi yake inabadilika kuwa nyeusi zaidi  na mafuta haya yanaanza kuharibika-Rancidity .
Nini uozo wa mafuta ya kupikia?
Uharibifu unatokana na uwepo wa hewa ya oksejini  hii inasababsha chembembe za mafuta kutengeneza kemikali za uchafu zinazojitokeza kwa mtiririko. Sababu zakutengenenza chemikali hizi pia zianchangiwa na vyombo vinavyotumika kuchemshia mafuta haya kama vile chuma (iron,zinc,copper, etc), chumvi, mwanga, maji, baketria na umbo la chombo kilicotumika kuchemshia mafuta.
Matatizo yanajitokeza unapoendelea kuchemsha mafuta
Kiasi cha sumu kinaongezeka kadri unavyo chemsha mafuta, sasa sumu hii ndio inayoleta tatizo kwenye afya. Kemikali nyingine kama vile polycyclic aromatic hydrocarbons zinaweza kujitengeneza kila mafuta yanapoendelea kuchemka jikoni. Baadhi ya mafuta ya mimimea kama karanga kwa mara moja moja inatengeneza baadhi ya sumu ambayo ni madhara kwa binadamu. Kwahiyo hata matumizi ya mafuta ya mimea yanamadhara makubwa kama yakiendelea kuchemshwa.
Matatizo ya kiafya
Mchemko wa mafuta hutengeneza kitu kama kutu  ambayo inaweza leta madhara kwa afya binadamu kwa sababu kutu hiyo hubaki katika mafuta, na mara nyingi huakisiwa na vyakula tutakavyo vikaanga na mara zote kumekuwa na viambata ambavyo hupatikana katika vyakula vilivyo kaangwa na mafuta yaliyo tumika sana. Matumizi ya mafuta hayo huwa huathiri ubora wa chakula kinacho kaangiwa au kupikiwa mafuta hayo.
Matumizi ya mafuta hayo hupunguza kiwango cha uyeyushaji wa chakula na usafirishaji chakula katika mishipa ya ndani ya damu na pia katika arteli na vishipa vidogo vya ndani ya moyo. Vyakula vyenye wingi wa mafuta ya kukaanga vilionesha kuwa na athari ya glukosi katika panya. Kuwemo kwa viambata kutu  katika mafuta ya kukaangia vimethibitika kusababisha matatizo ya shinikizo la damu., kisukari, figo na ini.

Ushauri...Nini tufanye
Tujaribu kutumia mafuta katika kukaanga kwa mara moja tu..tusiwe tunarudia kuchemsha mafuta. kaangia mara moja tupa kwa ajili ya afya yako.

No comments: